news

BAADA YA DABI KUISHA…KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA KWA MANULA..ADAI NI MAMBO YA MPIRA..

admin December 13, 2021 6:00 pm

 


NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mikono ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula iliwazuia kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi.

Juzi, Uwanja wa Mkapa, Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Simba lakini ubao wa ulisoma Simba 0-0 Yanga na kufanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.

Nabi amesema kuwa isingekuwa ni Manula basi wangeifunga Simba kwenye mchezo huo kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi ambazo zilikuwa zinawapa uhakika wa ushindi.

“Kipa wao yule wa Simba, (Aishi Manula) amefanya kazi kubwa kwenye kuokoa mipira yetu, kwa mfano kuna mpira ulipigwa na Said Ntibanzokiza unadhani asingekuwa imara nini kingetoa zaidi ya kuwa bao?

“Itoshe kusema kwamba ni kipa mzuri na ukitegemea kwamba ni kipa ambaye anadaka kwenye timu ya taifa, (Taifa Stars). Ni mambo ya mpira huwa yanatokea lakini ninawezakusema kwamba wachezaji wangu walicheza vizuri,” alisema Nabi.

Manula anafikisha jumla ya mechi nane kukaa langoni huku akiwa ameruhusu kufungwa mechi mbili mabao mawili na kwenye mechi sita alikuwa shujaa kwa kuwa hakufungwa.

BAADA YA KUWA KWENYE ‘SONGOMBINGO’ NA AZAM FC..YANGA WAMDAKA KININJA MUNATHIRI…ISHU IKO HIVI.. NABI AFUNGUKA KUHUSU MBINU ZA KOCHA MPYA SIMBA..ADAI NI BORA GOMES..” HUYU KAZI KUKABA TU”

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply