news

BAADA YA DABI…MAYELE ASHINDWA KUJIZUIA…’ATOA POVU’ KUKUMBATIWA KWA NYUMA NA INONGA…

admin December 14, 2021 1:29 pm

 


SHAMBULIAJI Mpya wa Yanga Mkongomani Fistoni Mayele, amesema kuwa yeye na Beki Mkongomani wa Simba Hennock Inonga ni washkaji wakubwa sana.

Wawili hawa wameiteka mitandao ya kijamii kwenye Dabi ya Kariakoo kutokana na jinsi ambavyo walipambana kwenye mchezo huo.

Inonga alionekana kumpania zaidi Mayele asiifunge timu yake, huku akisindikiza nje wakati anatoka uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Makambo.

Akizungumza na Championi Jumatatu Mayele amesema kuwa Inonga ni mshikaji wake mkubwa wana wanajuana muda mrefu “Inonga ni rafiki yangu sana na hatujawahi kucheza timu moja ila huwa tunakutana kwenye  majukumu ya timu ya Taifa.

“Mimi na yeye tunajuana sana na ni mshikaji wangu, hii ilikuwa kazi na ni lazima kila mmoja aonyeshe kiwango chake,” alisema mshambuliaji huyo.

UWANJA MPYA SIMBA ‘MAMBO NI MOTO’…UONGOZI WATOA TAMKO…WACHEZAJI WAHUSISHWA…. WAKATI YANGA WAKIENDELEA KUJITAFAKARI KISA SARE YA DABI…..SIMBA WAOGELEA MIHELA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply