Home news LICHA YA KUCHEZA VYEMA DHIDI YA YANGA…PABLO AIBUKA NA HILI DHIDI YA...

LICHA YA KUCHEZA VYEMA DHIDI YA YANGA…PABLO AIBUKA NA HILI DHIDI YA INONGA…


LICHA ya beki Mkongomani wa Simba, Henock Inonga Baka kuonyesha kiwango bora katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Yanga, Kocha mkuu wa Simba, Pablo Franco amewaambia Wanasimba watulie wataona makubwa zaidi kutoka kwa nyota huyo.

Simba juzi Jumamosi wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam walilazimishwa suluhu na Yanga katika mchezo wa Kariakoo Dabi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Katika mchezo huo, Inonga alionekana kuwa kwenye kiwango bora zaidi akipiga pasi 31 zilizofika kati ya 34, huku pia akifanikiwa kushinda mipira sita ya juu dhidi ya mastraika wa Yanga.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Pablo alisema: “Nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wangu kwa kucheza vizuri kulingana maelekezo tuliyowapatia ni wazi ulikuwa mchezo mgumu na mzuri kwa pande zote mbili, jambo la muhimu kwetu ni kwamba tumepata pointi moja na tunaendelea kusalia nafasi ya pili.

“Najua watu wengi kwa sasa wanamzungumzia Inonga kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha, lakini kwangu wachezaji wote wa Simba walicheza vizuri hasa kutokana na ukweli kuwa wapinzani wetu walipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, lakini hata huyo Inonga kuna vitu tutamuongezea na atakuwa bora zaidi.”

SOMA NA HII  YANGA KURUDI KIVINGINE LIGI KUU, CAF.....MABOSI 'WAPIKA NA KUPAKUA DIKO' LA KWENDA...