news

PAMOJA NA KUONGOZA LIGI..NABI AFUNGUKA KUTOFURAHISHWA NA YANGA..ADAI HAICHEZI VIZURI…

admin December 14, 2021 8:00 am


KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi ametamba kwa jinsi timu anavyoitengeneza, basi wanachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo alitoa kauli hiyo mara baada ya Kariakoo Dabi kumalizika kwa suluhu. Dabi hiyo iliwakutanisha Simba dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, juzi Jumamosi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nabi alisema kuwa licha ya timu yake kusifiwa na soka safi la pasi, lakini anahitaji muda zaidi wa kuendelea kukiboresha kikosi chake. Nabi alisema kuwa jinsi anavyotaka timu yake icheze, basi ngumu kukosa ubingwa msimu huu.

Aliongeza kuwa hakuna kitakachoshindikana kwake kutokana na ubora wa kikosi chake.

“Kwa jinsi ambavyo ninataka timu yangu icheze, hakuna kitakachoshindikana kwangu kubeba ubingwa.

“Ninafurahia kuona timu yangu inavyocheza, lakini bado sijafurahia vile ninavyotaka.

“ Ninaamini hivi karibuni mashabiki wa Yanga watafurahia zaidi kwa jinsi soka ambalo ninataka kuona wakicheza vijana wangu.

“Niwaondoe hofu Wanayanga kuwa ubingwa tunachukua msimu huu. “ Nafahamu Wanayanga wana hamu ya ubingwa baada ya kuukosa kwa miaka minne,”alisema Nabi.

LICHA YA KUCHEZA VYEMA DHIDI YA YANGA…PABLO AIBUKA NA HILI DHIDI YA INONGA… BAADA YA VIKAO VIIINGI…HATIMAYE CHAMA HUYU HAPA..WAMOROCO WAKUBALI YAISHE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply