Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…SIMBA WALIA…GONJWA LA AJABU LAVAMIA ROBO TATU YA WACHEZAJI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…SIMBA WALIA…GONJWA LA AJABU LAVAMIA ROBO TATU YA WACHEZAJI…


Kocha Msaidizi wa timu ya Simba, Selemani Matola amesema kuwa karibia robo tatu ya wachezaji wa timu hiyo wanakabiliwa na ugonjwa wa mafua, kifua pamoja na homa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mkoani Kagera Matola amesema wachezaji wengi wanakabiliwa na ugonjwa huo ambao haujulikani chanzo chake ingawa madaktari bado wanafanya vipimo mbali mbali kujua chanzo

“Nashkuru Mungu tumeweza kufika salama jana japokuwa tumekuwa na changamoto kidogo baadhi ya wachezaji nafikiri karibu robo tatu wamekuwa wakiugua mafua na kifua na homa za hapa na hapa sijui ni kutokana na hali ya hewa au ni nini na baadhi ya benchi la ufundi” amesema Matola na kuongeza

“Mpaka sasa hatujui itakuwaje kwani hatujui chanzo na tumeacha madaktari wafanye vipimo na baadae tujue nini tatizo kwani hata mimi na baadhi ya watu wa benchi la ufundi wanaumwa”

Kwa upande wake Francis Baraza ambae ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema timu Yake pia inakabiliwa na tatizo hilo kwani daktari wa timu na kocha Msaidizi wanaumwa

“Hili tatizo pia kwetu lipo tumetokea kwenye mchezo dhidi ya Azam baadhi ya watu wa benchi akiwemo daktari na kocha msaidizi wanaumwa nadhani ni suala la mabadiliko ya hali ya hewa”. amesema Baraza

Simba watamenyama na Kagera Sugar hapo kesho Desemba 18 katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

SOMA NA HII  MAJINA MATATU NYOTA WA SIMBA YAPITISHWA KUWANIA TUZO