Home news YANGA MAMBO YAZIDI KUWA ‘BAMBAM’…KUANZIA MWAKANI KUANZA KUVUNA MABILIONI YA UWEKEZAJI….

YANGA MAMBO YAZIDI KUWA ‘BAMBAM’…KUANZIA MWAKANI KUANZA KUVUNA MABILIONI YA UWEKEZAJI….


BAADA ya wanachama wa Yanga chini ya Mwenyekiti wao Mshindo Msola kupitisha mabadiliko ya Katiba Serikali imeungana nao kwa kuipitisha rasmi.

Wanachama wa Yanga Juni 27 mwaka jana waliunga mkono mabadiliko hayo katika mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa DYCC, Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo juzi Alhamis imethibitisha kuwa katiba yao imesajiliwa rasmi na Serikali.

Taarifa hiyo ilisema uongozi unawataarifu wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau kwamba katiba mpya ya klabu ya mwaka 2021 imesajiliwa rasmi na Serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ofisi ya msajili wa vyama na klabu za michezo nchini.

“Kukamilika kwa usajili wa katiba mpya ya klabu kama ilivyopitishwa na mkutano mkuu wa wanachama Juni 27 kuna ruhusu mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kama ambayo imeainishwa kwenye mabadiliko ya katiba ya mwaka 2021,” ilisema taarifa hiyo.

SOMA NA HII  UHAKIKA....MORRISON KUTUA SINGIDA BIG STARS....ISHU YA PHIRI KUMBE NI 'VIJIMANENO' TU...