News

BAADA YA KUZUIWA KUINGIA UWANJANI NA PABLO..WAWA AVUNJA UKIMYA ..AFUNGUKA YANAYOENDELEA…

admin December 26, 2021 7:00 pm


PASCAL Wawa, beki wa kati wa Simba, ameweka wazi kuwa hakuna tofauti kati yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco.

Juzi, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ilitokea hali ya kutoelewana katika suala la kufanya mabadiliko ambapo Wawa alikuwa anajiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi ghafla, Pablo alimvuta kwa nguvu kubwa na kuonekana akilalamika.

Pia Pablo alionekana mwenye hasira ambapo alionekana akipiga kiti na chupa ya maji jambo ambalo liliweza kuonesha kwamba alikuwa amekasirika kwelikweli.

Kutokana na kitendo hicho ilibidi Wawa arudi benchi na kumaliza dakika 90 akishuhudia mchezo huo ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma KMC 1-4 Simba.

Wawa amesema kuwa hakuna tofauti kati yake na kocha wa timu hiyo.

“Hakuna tofauti kati yetu na kocha kila kitu kinakwenda vizuri na tunashukuru kwa kuwa tumeshinda,” alisema Wawa.

RASMI..MTIBWA SUGAR YAMALIZANA KIBABE NA DEO KANDA…ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI… IMEFICHUKAA…HIVI NDIVYO USAJILI WA  ‘SURE  BOY’ ULIVYOIKAMUA YANGA MAMILIONI YA PESA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply