news

KUHUSU ISHU YA CHAMA KUTUA SIMBA…BARBARA AAMUA KUFANYA KWELI…APANDA NDEGE MPAKA MOROCCO..

admin December 27, 2021 7:00 pm

 


VIGOGO wa Kamati ya Usajili ya Simba, chini ya Mtendaji Mkuu (C.E.O.) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez, wameona isiwe shida na kuchukua maamuzi ya kupanda ndege kumfuata kiungo wao mchezeshaji Mzambia Clatous Chama anayekipiga RS Berkane ya nchini Morocco.

Kiungo huyo anawindwa vikali na Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho.

Simba imepanga kukiboresha kikosi hicho katika dirisha dogo ambalo inaelezwa tayari imemalizana na winga wa Zanaco, Mzambia Moses Phiri.Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa haraka mabosi wa Simba wamechukua maamuzi ya kumfuata Chama Morocco kwa ajili a kufanikisha dili lake.

Bosi huyo alisema kuwa tayari uongozi huo ulishafanya mazungumzo na wazazi wa Chama walipokwenda kucheza mchezo wa Kombe la ShirikishoAfrika dhidi ya RedArrows ya nchini Zambia.

“Mazungumzo yetu na Chama yanakwenda vizuri, mtendaji wetu Barbara na baadhi ya viongozi wa kamati ya usajili wapo safarini kuelekea Morocco kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

“Dili hilo muda na wakati wowote litafanikiwa, kwani viongozi hao wapo Morocco kwa ajili ya kuzungumza na Berkane iliyomsajili katika msimu huu.

“Safari hiyo ya Barbara haitaishia kwa Chama pekee kwani pamoja na kuwepo kwa dili hilo, tayari kuna nyota mwingine ambaye ni kiungo mkubwa tu anaweza kutua kwa ajili ya kuziba pengo la Lwanga kipindi hiki ambacho yeye ana majeraha ya goti ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu,” alisema bosi huyo.

Simba kwa kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa timu hiyo, SalimAbdallah ‘Try Again’ilisema: “Sisi Simba ndiyo wenye nafasi kubwa ya kumsajili Chama, kwani katika mkataba wake kuna masharti tuliyokubaliana nayo ambayo kama ataachana na Berkane, basi Simba ndiyo tutapewa kipaumbele.”

WAKATI ISHU YA CHAMA NA PHIRI IKIWA HEWANI BADO…PABLO AMALIZA KILA KITU SIMBA..MAGORI ATEMA CHECHE.. BAADA YA KUISHUHUDIA SIMBA IKIIUA KMC..PABLO ATIKISA KICHWA ..ASISITIZA MAMBO BADO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply