news

BREAKING….MSHERY RASMI MALI YA YANGA…APEWA JEZI KUBWA KULIKO UMRI WAKE….

admin December 29, 2021 3:41 pm


KIPA namba moja wa Mtibwa Sugar, Aboutwaleeb Mshery (21) leo Desemba 29 amemalizana na vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Mshery amejiunga na Yanga, tayari kwa ajili ya kuziba pengo la kipa namba moja wa timu hiyo Djigui Diarra ambaye ameenda Mali kwenye majukumu ya timu ya taifa wanaojiandaa na michuano ya Afcon.

Kipa huyo tayari amewasili kambi ya Yanga, iliyopo Avic Town Kigamboni, ambako alitambulishwa mbele ya wachezaji wenzake, wakati wa mazoezi, kisha akarudi kwenye gari alilokuja nalo.

Baadae Mshery alibadilisha nguo na kuvaa jezi na kwenda kujiunga na wenzake mazoezini katika programu ya kocha Nabi.

Kipa huyo tayali amepewa jezi namba 50 mgongoni ambayo inanamba kubwa kuliko umri wake, na kupewa glavu tayari kwa ajili ya mazoezi.

Yanga wameanza mazoezi ya kuelekezwa kwa kutumia ubao wakiwa wamekaa chini na kocha Nabi akiwa anawaelekeza kwa kuandika.

BAADA YA KUSAINI  TU …’SURE BOY’ APEWA JEZI YENYE GUNDU ..KILA ALIYEIVAA HAKUDUMU NA YANGA.. BAADA YA TETESI KUWA NYINGI…MBEYA KWANZA WAVUNJA UKIMYA DILI LA NGUSHI KUTUA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply