news

PAMOJA NA KUJIKAKAMUA KOTE KULE…PABLO AMFUNGIA VIOO MAZIMA AJIB…NAYE KUSEPESHWA SIMBA…

admin December 30, 2021 4:00 am


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC huenda wakamtoa kwa mkopo Kiungo Ibrahim Ajib, katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Ajibu anatajwa kuingia kwenye mpango huo, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza chini ya Kocha Franco Pablo Martin ambaye amerithi mikoba ya Didier Gomes.

Hata hivyo bado haijafahamika ni wapi kiungo huyo atapelekwa kwa mkopo, lakini taarifa zinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka Msimbazi.

Wachezaji wengine wanaotajwa huenda wakatolewa kwa mkopo ni Mlinda Lango Jeremiah Kisubi na Kiungo na Abdulsamad Kassim, ambao pia wamekosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Simba SC bado ipo kimya katika usajili wa wachezaji, huku ikielezwa kuwa huenda wakaweka wazi kila kitu baada ya kufanikisha mpango wa kuwatoa baadhi ya wachezaji wao kwa mkopo.

TULIENI..TUNATOBOA..MABOSI SIMBA WAAPA..WALITAJA CHAMA LA KISINDA..MWANASPOTI LEO.. BAADA YA KUCHUKUA STRAIKA WA YANGA…DODOMA JIJI YATUA SIMBA…YABEBA STRAIKA WAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply