Home news BAADA YA KUWA KWENYE ‘SONGOMBINGO’ NA AZAM FC..YANGA WAMDAKA KININJA MUNATHIRI…ISHU IKO...

BAADA YA KUWA KWENYE ‘SONGOMBINGO’ NA AZAM FC..YANGA WAMDAKA KININJA MUNATHIRI…ISHU IKO HIVI..


YANGA wamepania kukiongezea makali kikosi chao hasa eneo la kiungo ambapo inatajwa kuwa wamemalizana na kiungo Mudathir Yahya wa Azam FC.

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao walisimamishwa na Azam FC kwa kipindi kisichojulikana, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu dhidi ya uongozi na benchi la ufundi la kikosi cha timu hiyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimesema kuwa Jumamosi kuwa uongozi wa Yanga tayari umekamilisha dili hilo, baada ya kujiridhisha juu ya matakwa ya mchezaji huyo ya kutohitaji kusalia ndani ya Azam na sasa linasubiriwa dirisha la usajili kufunguliwa ili dili hilo liwekwe wazi.

“Ni kweli tumekamilisha mazungumzo ya usajili wa kiungo Mudathir Yahya kutoka Azam, hii ni baada ya kujiridhisha juu ya maamuzi ya mchezaji husika kutohitaji kuendelea kusalia ndani ya kikosi chao kutokana na changamoto ya kimahusiano na uongozi wa juu wa klabu hiyo.”

Akizungumza kuhusu masuala ya usajili ndani ya Yanga, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela alisema: “Mipango yote ya usajili wa dirisha dogo kwenye kikosi chetu inaendelea vizuri, na tunachosubiri kwa sasa ni kufunguliwa rasmi kwa dirisha la usajili ili kuanza kutangaza rasmi wachezaji wote ambao tumemalizana nao.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SHOW YA YANGA JANA...KMC 'WAMEZA MATE KWA UCHUNGU' KISHA WAKASEMA HAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here