Home news KISA DIARRA..YANGA YAMVUTIA KASI MAKAKA WA RUVU SHOOTING…MPANGO MZIMA UKO HIVI..

KISA DIARRA..YANGA YAMVUTIA KASI MAKAKA WA RUVU SHOOTING…MPANGO MZIMA UKO HIVI..


Mabosi wa Yanga wanafikiria uwezekano wa kumpata mlinda lango wa Ruvu Shooting Mohammed Makaka kuchukua nafasi ya kipa namba moja wa klabu hiyo Diarra Djigui ambaye anatarajiwa kuwa kwenye majukumu na timu yake ya taifa kwenye michuano ya AFCON mwezi Januari.

Yanga pia inampigia hesabu kipa wa Mbeya City Haroun Mandanda endapo watamkosa nyanda huyo wa maafande wa Ruvu Shooting.

Djigui aliyesaliwa msimu huu kutoka Stade Malien ya kwao Mali, ni mmoja ya makipa watakaoenda katika Fainali za Kombe la Afrika (Afcon) 2022, hivyo Yanga huenda ikabakia na kipa mmoja tu, Erick Johora huku Ramadhani Kabwili akipigwa chini mapema.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA JUMAMOSI HII...SURE BOY 'AMNG'ATA SIKIO' NABI....ALILIA KUKIVURUGA PALE KATI...