Home news KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…LWANGA NA MUGALU ‘OUT’ SIMBA…PABLO AKATAA VISINGIZIO…ADAI HAIWEZEKANI…

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…LWANGA NA MUGALU ‘OUT’ SIMBA…PABLO AKATAA VISINGIZIO…ADAI HAIWEZEKANI…


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Pablo Franco Martin amethibitisha atawakosa wachezaji Chris Mugalu na Thadeo Lwanga katika mchezo wa keshokutwa Jumamosi (Desemba 11).

Simba SC itakua mwenyeji wa Young Africans, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam katika mchezo wa mzunguuko wanane wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema kukosekana kwa wachezaji hao kwake ni ‘pigo kubwa’, lakini ameahidi haitawazuia kupambana na kufikia lengo la kupata alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Amesema alihitaji kuona wanatumia uzoefu wao wa michezo ya Kimataifa ili kuongeza nguvu, lakini tayari ameshapata nyota wengine ambao amewaandaa kuonyesha kiwango kizuri.

“Nimetoka kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika na kutinga hatua ya makundi, hivyo ningehitaji siku nyingine tatu za maandalizi, lakini haiwezekani.”

“Nakwenda kuwakosa wachezaji wangu muhimu (Thadeo Lwanga na Chris Mugalu) katika mchezo huo, sitaki visingizio, tutapambana ili tushinde mchezo huo, tupate alama tatu na nina imani tutashinda, ingawa wapinzani wetu ni wazuri na wana wachezaji wazuri pia,” amesema Pablo.

Simba inakwenda kucheza mchezo huo ikiwa na kumbukumbu kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kuwnaia Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 25, mwaka huu.

Lakini itakuwa ni ‘dabi’ ya kwanza ya Pablo tangu ajiunge na timu hiyo mwezi uliopita, ikiwa ni mchezo wake watano wa mashindano. Tayari ameshaiongoza Simba kwenye michezo minne, miwili ya kimataifa na miwili ya Ligi Kuu, akishinda mitatu na kupoteza mmoja.

Michezo miwili ni ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia ya nyumbani na ugenini ikishinda mabao 3-0 nyumbani na kufungwa mabao 2-1 Lusaka, huku ikiwa imecheza michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting ikishinda mabao 3-1 na Geita Gold ikishinda mabao 2-1.

SOMA NA HII  YANGA HALI TETE LIGI YA MABINGWA ALLY KAMWE ATOA KAULI TATA