Home kimataifa DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA

DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA


 UONGOZI wa Klabu ya Barcelona umeweka wazi kuwa upo kwenye mpango wa kujiandaa kukutana na mwakilishi wa nyota wao Ousmane Dembele.

Kwa mujibu wa Rais wa Klabu ya Barcelona inayoshiriki La Liga, Joan Laporta amesema kuwa wapo kwenye hesabu za kufanya mazungumzo na mwakilishi wa staa huyo ili waweze kukamilisha ishu ya kuongeza mkataba mpya.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa Barcelona wanataka kukutana na mwakilishi wa Dembele ili aweze kusaini dili jipya kwa kuwa kandarasi yake kwa sasa imebakiza miezi 12 pekee.

Ni jezi namba 7 ambayo amepewa staa huyo ambayo awali ilikuwa ikitumiwa na Antoine Griezmann ambaye kwa sasa amejiunga na Klabu ya Atletico Madrid lakini bado Dembele kwa sasa hajaanza kukipiga kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

“Naamini kuwa tutamaliza kila kitu hivi karibuni atakubali kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu yetu,” amesema rais huyo. 

SOMA NA HII  MANARA 'APIGILIA NYUNDO' ISHU YA MAYELE KUTAKIWA KAIZER CHIEF...ATUPA DONGO SIMBA...