Home Uncategorized COASTAL UNION YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU ALI KIBA

COASTAL UNION YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU ALI KIBA


KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa kwa sasa hawafikirii kumuacha mchezaji Ali Kiba licha ya kuwa na majukumu mengi kwani uwezo wake ni wa juu.

Akizungumza na Salehe Jembe, Mgunda amesema kuwa msimu uliopita Kiba alishindwa kuonyesha uwezo wake kutokana na kubanwa na ratiba hivyo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo naye ili kujua namna atakavyoihudumia kwa ukaribu.

“Kiba ni miongoni mwa wachezaji wazuri, bado ni mali ya Coastal Union kwa kuwa tulimsajili kwa malengo, hivyo kwa sasa tunatazama namna rafiki itakayofaa kuendelea kutumika ndani ya kikosi chetu,” amesema.

SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI PASUA KICHWA KWA ZAHERA WA YANGA