Home news KUELEKEA MAPINDUZI CUP…YANGA WAPANGA KUFANYA ‘SAPRAIZI’ YA KARNE…MAKUSU NDANI…

KUELEKEA MAPINDUZI CUP…YANGA WAPANGA KUFANYA ‘SAPRAIZI’ YA KARNE…MAKUSU NDANI…


RASMI uongozi wa Yanga umefunguka kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo katika dirisha hili dogo la usajili kutumika katika michuano ya Kombe la Mapinduzi itayoanza kutimua vumbi Januari visiwani Zanzibar.

Yanga katika dirisha hili dogo la usajili wanahusishwa kwa karibu na baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji Jean Marc Makusu anayekipiga DC Motema Pembe na kiungo mshambuliaji Fabrice Ngoma anayekipiga Raja Casablanca ya Morroco.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliweka wazi kuwa timu hiyo itafanya usajili wa wachezaji kupitia dirisha hili dogo la usajili ambapo katika usajili huo wapo ambao watatumika katika michuano ya Mapinduzi na wengine hawatatumika katika michuano hiyo kulingana na matakwa ya timu.

“Yanga kupitia dirisha dogo la usajili lazima tutafanya usajili wa wachezaji ambapo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa ligi dhidi ya Biashara United, basi tutaelekea katika Kombe la Mapinduzi ambapo kuna wachezaji ambao tutawasajili wataitumikia timu katika michuano.

“Yanga kwa sasa kuna wachezaji wengi ambao ni majeruhi kama Fiston Mayele, Yacouba Songne, Yusuph Athuman, Kibwana Shomari hivyo lazima kufanyike usajili kwa baadhi ya maeneo kulingana na wapo ambao watakosekana kwa muda mrefu na hivi karibuni maingizo mapya yatajulikana.

“Wachezaji wote ambao watasajiliwa watajulikana na uongozi wa Yanga na benchi la ufundi ndio unafahamu ila hao ambao unawasikia sio rasmi kutoka kwetu,” alisema Bumbuli.

SOMA NA HII  TFF YATOA TAMKO ISHU YA KUONGEZA MUDA DIRISHA LA USAJILI