Home Uncategorized KAGERA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA

KAGERA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA

MECKY Mexime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wapinzani wake Simba wapo vizuri ila wao hawana hofu na hilo.

Kagera Sugar leo itakuwa kazini Uwanja wa Taifa kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa mzunguko wa pili.

Mexime amesema:”Tunacheza na timu ambayo ipo imara na ina mwendo mzuri hilo tunalitambua ila halitufanyi tuwe na hofu juu yao kwani nasi tupo pia vizuri, wachezaji wanatambua majukumu yao watapambana uwanjani kupata matokeo,”.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba kwa msimu wa 2019/20 Kagera Sugar ilalala kwa mabao matatu na kuifanya Simba isepe na pointi uwanja wa Kaitaba.

SOMA NA HII  UJUMBE WA JEMBE KWA NADIR HAROUB WA YANGA