Home news SIMBA DAY KUPIGWA AGOSTI 6, AHMED ALLY ATAMBA

SIMBA DAY KUPIGWA AGOSTI 6, AHMED ALLY ATAMBA

TAMASHA la ‘Simba Day’ mwaka huu litafanyika rasmi Agosti 6 badala ya Agosti 8 kama ambavyo imezoeleka kila msimu kwenye timu ya Simba.

Tamasha hilo ambalo limekuwa kubwa na maarufu nchini limepangwa kufanyika Agosti 6 kutokana na ratiba kubana ndani ya kikosi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema sababu ya kurudisha nyuma tamasha hilo ni kutokana na ugumu wa ratiba.

“Agosti 10 tutakuwa na mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fontain Gate kule Tanga hivyo tumeona ni vyema kurudisha nyuma siku mbili ili tuwape wachezaji mapumziko, naamini tunaweza kufanya vizuri katika hiyo mechi.”

Tamasha hilo litakuwa ni la 15 tangu lilipoanzishwa mwaka 2009 na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali na katibu wake, Mwina Kaduguda.

SOMA NA HII  BAADA YA THANK YOU ZA KUTOSHA SIMBA, SASA NI ZAMU YA KAPOMBE