Home Habari za michezo ISHU YA CHAMA KWENDA YANGA IMEBAKI STORI, SIMBA WAZIMA NGOMA KIBABE

ISHU YA CHAMA KWENDA YANGA IMEBAKI STORI, SIMBA WAZIMA NGOMA KIBABE

ishu ya Clatous Chama na Simba ni kama imeisha na muda wowote kiungo huyo atarejea mzigoni.

Chama alitingisha kutaka kutimka klabuni hapo kwa kile alichodai mkataba wake ulishamalizika na tayari ameshapata timu na ndipo Simba walipojiridhisha kwamba wakimuachia tu anatua Yanga.

Mabosi wa Simba walishajua anachotaka na haraka wakaingiza fedha za ada ya usajili ambazo zilikuwa zimesalia kwenye mkataba wa mwaka mmoja ulioko kwenye mamlaka za Soka, bila yeye kujua.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba Chama alitakiwa kulipwa fedha hizo kabla ya msimu ujao kuanza ambapo haraka wakaingiza fedha hizo Julai 13 kwenye akaunti yake na alipokwenda mezani akakutana na risiti ambayo ilimuweka kwenye mtihani mkubwa.

Kuingizwa kwa fedha hizo kumemuacha njia panda Chama kuendelea na msimamo wake kwa kuwa tayari Simba imeshakamilisha makubaliano yao ya kimkataba na mkataba.

Sakata hilo liliwaweka Yanga katika mkao wa kula wakisubiri hatma yao ambapo Mwanaspoti linafahamu kuwa tayari mabosi wa Yanga walishampigia simu wakimuandalia mkataba kwa sharti la kumalizana kwanza na klabu yake.

Hii inamaanisha kwamba uwezekano wa Yanga kumpata Staa huyo umeyeyuka kwani mkataba unaosoma kwenye mamlaka za Soka unambana na fedha aliyotaka ameshalipwa.

SOMA NA HII  ZORBAS TAVERN SLOT YA KUANZA MWAKA 2024 KWA MKWANJA WA UHAKIKA KUTOKA MERIDIANBET..