Home news WAKATI YA PHIRI NA CHAMA YAKIWA TAYARI…SIMBA WATUPA TENA NDOANO ZAMBIA..SAFARI HII...

WAKATI YA PHIRI NA CHAMA YAKIWA TAYARI…SIMBA WATUPA TENA NDOANO ZAMBIA..SAFARI HII NI SIKAONGA…


KIUNGO mkata umeme wa Zesco ya nchini Zambia, Samuel Sikaonga, ameweka wazi kuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Klabu ya Simba wametuma ofa wakitaka ajiunge nao.

Mbali na Simba, Sikaonga amesema pia Azam FC wametupa ndoano kwake wakitaka ajiunge nao kwenye dirisha dogo lililofunguliwa juzi Jumatano. 

Kiungo huyo mkabaji mwenye miaka 22, ameliambia ChampioniIjumaa kuwa, amepewa taarifa na viongozi wake kuwa Simba na Azam FC zinamtaka na yeye yuko tayari kujiunga na timu moja wapo itakayokuwa na ofa nzuri.

“Ni kweli nimeambiwa na uongozi wangu kuwa Simba na Azam wananihitaji na mimi nipo tayari kuweza kujiunga nao, maana Simba ni timu nzuri pia Azam ni wazuri ni suala la muda,” alisema kiungo huyo ambaye ana mkataba wa miaka miwili Zesco.

Akizungumzia ishu ya usajili, Simba kupitia Kocha Msaidizi wao, Thierry Hitimana alisema kuwa:

“Najua kuna wachezaji lazima wataongezwa ila mpaka sasa bado sijaambiwa ni nani na nani nafikiri kocha mkuu, Pablo (Franco) ataongea na uongozi ilo suala la usajili tutaliweka wazi baadaye.”

SOMA NA HII  UCHAGUZI MKUU SIMBA:..MWANACHAMA 1000 TU KUPIGA KURA LEO...MAMBO YA KUZINGATIA HAYA HAPA...