news

KISA MANULA….SHABIKI ATOZWA FAINI YA TSH ELFU 20…KOCHA AKOMALIA KISHA ADAI UTANI….

admin January 1, 2022 2:30 pm


KATIKA hali isiyotarajiwa, kwenye mazoezi ya Simba, kocha mpya wa makipa wa timu hiyo raia wa Afrika Kusini, Tyron Damos, alimkamata shabiki mmoja akirekodi mazoezi aliyokuwa akimpa kipa wake Aishi Manula na kuamuru shabiki huyo alipe faini ya Sh 20,000.

Kwenye mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO arena, Bunju Dar es Salaam, Simba waliruhusu watu mbalimbali kurekodi mazoezi hayo kwa dakika 15 tu kabla ya kuzuia kurekodi mazoezi ya kimbinu.

Licha ya zuio hilo shabiki mmoja aliendelea kurekodi na kumfanya kocha huyo Msauzi kumshtukia ambapo alisimamisha mazoezi na kumfuata shabiki huyo na kumwambia anapaswa kulipa faini ya Sh 20,000 kwa kukiuka maelekezo.

Tyron alisikika akisema akisema: “Nimekuona ulikuwa ukirekodi programu zetu za kiufundi nilizokuwa nampa Manula na kwa kuwa hiyo ni kinyume cha maelekezo basi utapaswa ulipe faini ya shilingi 20,000.”

Mwishoni kocha huyo alianza kutabasamu na kumwambia shabiki aliyekuwa akirekodi kuwa alikuwa anamtania, na kumtahadharisha kuwa asiendelee kufanya hivyo.

KUELEKEA MICHUANO YA CAF…KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YA KIMAFYA..WAZITAKA MECHI MBILI.. WAKATI YANGA NA GSM WAKITAKA KUMPA MIL 400 …HIVI NDIVYO MO DEWJI ALIVYOFANYA KUFURU ISHU YA CHAMA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply