news

KUHUSU HATMA YA YACOUBA YANGA….KAZE AVUNJA UKIMYA…AGUSIA ISHU YA MSHAMBULIAJI MPYA….

admin January 1, 2022 5:00 pm


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema mshambuliaji, Yacouba Songne bado ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa sababu bado ana nafasi katika kikosi cha timu hiyo licha ya kusajili wachezaji wengine wapya wa kimataifa.

Kaze ametoa kauli hiyo ni baada ya kuwapo kwa tetesi Songne jina la nyota huyo linaweza kuondolewa ndani ya kikosi cha Yanga kutokana kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Kaze alisema kwa sasa hawana mpango wa kumwondoa moja kwa moja nyota huyo kikosini kwa sababu wanafahamu bado anauguza majeraha lakini wanathamini kiwango chake.

Alisema mchezaji huyo ataendelea kubaki ndani ya kikosi cha Yanga huku akifanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari mpaka pale hali yake itakapoimarika.

“Tukiwa tunaendelea kutafuta mshambuliaji mwingine kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji, lakini uamuzi wa kutafuta mshambuliaji mwingine hautaleta maana Yacouba anaondolewa kwenye mipango yetu moja kwa moja,” alisema Kaze.

Alisema wanaamini mara mshambuliaji huyo atakapopona, atarejea kwenye kikosi na kuisaidia timu hiyo ifikie malengo yake.

BAADA YA KUTOPEWA NAFASI…MUKOKO SHINDWA KUJIZUIA YANGA…AFUNGUKA ANAYOPITIA… FT: SIMBA 2-1 AZAM FC…..KANOUTE ALIAMSHA …SAKHO AWAVURUGA…VARANE ACHAPWA KOFI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply