news

WAKATI WATU WAKIMTAJA TAJA CHAMA..TRY AGAIN AIBUKA NA HILI..AMTAJA MIQUISSONE….

admin January 3, 2022 6:00 pm


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’, amesema mipango ya Simba kwa sasa ni kutawala soka la Afrika na kutetea ubingwa.

Try Again alifunguka kuwa timu hiyo kwa sasa ina mwenendo mzuri baada ya mechi chache na mambo yanavyokwenda atakuja kuonekana mrithi sahihi wa Luis Miquissone kutokana na kuimarika kwa wachezaji kadhaa kwenye timu hiyo.

Akizungumza hivi karibuni, Try Again alieleza kuwa wanataka kulishika soka la Afrika na ndiyo maana wamekuwa makini sana kwenye kutafuta wachezaji ambao wataitumikia timu hiyo kwa sasa na dalili za sasa zinaonyesha kuwa wanakwenda kulitimiza hilo.

“Tunakwenda kuliteka soka la Afrika, hiyo ndiyo mipango yetu, timu sasa imeanza kuimarika na kuna wachezaji nyota wameanza kuonyesha kuwa wao ni wa levo nyingine kabisa, tutawaona kina Miquissone wapya muda siyo mrefu.

“Tupo makini kwenye kufanya usajili lengo kubwa ni kuwa na timu imara zaidi itakayotikisa kwenye levo za kimataifa,” alisema Try Again.

SIMBA YA MO DEWJI NI BABA LAO..YAIZIDI UJANJA YANGA YA GSM..WAMALIZANA NA BEKI KITASA CHA KAZI…. RASMI..MASHINE MBILI ZATUA SIMBA..PABLO SASA ATANGAZA VITA..NABI AWAVAA MABOSI YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply