news

KUHUSU USAJILI MPYA…SIMBA KUJA NA SAPRAIZI…DEWJI AWAKATAA KINA SHIBOUB..TRY AGAIN AMTAJA CHAMA…

admin January 8, 2022 7:18 am


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema klabu hiyo imefunga usajili wao msimu huu.

Amesema watamtambulisha nyota mpya kutoka nje ya nchi ambaye ndiye amewafungia usajili wao wakati huu wa dirisha dogo.

“Tayari tumekwishamaliza naye, ila sitomtaja jina na nchi anayotoka sababu utamfahamu, lakini tumemalizana naye na hivi karibuni atatambulishwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Try Again (Salim Abdallah),” amesema Dewji.

Hivi karibuni Simba kwenye mkutano mkuu ilifichua kuwa na mpango wa kumrejesha Cleotus Chama.

Katika hotuba yake, Try Again alisema watamrejesha mchezaji huyo jambo ambalo lilishangiliwa na mamia ya wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam.

Kuhusu wachezaji waliokuja nchini kwa ajili ya majaribio kwenye timu hiyo, Kassim Dewji amesema hakuna hata mmoja atakayesajiliwa na klabu hiyo msimu huu.

“Mawakala wao ndiyo waliomba waje kufanya majaribio, kama klabu hatukuona sababu ya kuwakatalia, lakini kama nilivyosema hakuna hata mmoja ambaye atasajiliwa kati yao kwenye timu yetu,” amesema.

MKE AINGILIA KATI SAKATA LA FRAGA KURUDI SIMBA…ATOA MASHARTI MAZITO KWA UONGOZI… PAMOJA NA KUCHEZA JUZI….PABLO ADAI HAMJUI NA HAJAWAHI KUMUONA SHIBOUB…AGUSIA HATMA YAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply