news

MORRISON BANA…PAMOJA NA KUWA NA VITUKO VINGI VYA KUKERA…KUMBE ‘SOMETIME YES’…

admin January 10, 2022 12:00 pm


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison, amefunguka kwamba, kwa sasa anajipanga kuhakikisha anaisaidia timu yake kushinda mechi ya nusu fainali na kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Kauli ya Morrison imekuja baada ya Simba kumaliza kinara wa Kundi C ikikusanya pointi nne katika michuano hiyo inayoendelea Zanzibar na kutinga nusu fainali ikitarajiwa kucheza na Namungo, leo Jumatatu.

Katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliochezwa juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan, Simba ilishindwa kufungana na Mlandege.

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema kuwa: “Mlandege ni timu nzuri, hii sio mechi yetu ya kwanza kukutana, huko nyuma tushawahi kucheza nao, ni timu yenye ushindani mkubwa sana.

“Tulijitahidi kuhakikisha tunapata ushindi, lakini tumeukosa. Kwa sasa tunaangalia hatua inayofuata ya nusu fainali ambayo tutahakikisha tunashinda na kuingia fainali kwenda kuchukua ubingwa.”

PAMOJA NA KUWA KWA SASA HATAJWI TAJWI SANA…MAKAMBO AZIDI KUKIMBIZA MWIZI KIMYA KIMYA… HUU HAPA MTAZAMO WA MAKOCHA WA ULAYA KUHUSU UWEZO WA KIBU..WADAI ANA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply