Home news AISEEE…HUYO NOVATUS ANAVYOKICHAFUA HUKO ISRAEL NI MUNGU TU ANAJUA…’ATUPIA GOLI TAKATIFU’…

AISEEE…HUYO NOVATUS ANAVYOKICHAFUA HUKO ISRAEL NI MUNGU TU ANAJUA…’ATUPIA GOLI TAKATIFU’…


KIUNGO Mtanzania, Novatus Dismas ametupia bao moja na kuibeba timu yake ya Beitar Tel Aviv kuvuna pointi moja kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Israel ‘Liga Leumit’ dhidi ya Hapoel Kfar Saba ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Beitar Tel Aviv ambayo anaichezea Novatus kwa mkopo akitokea Maccabi Tel Aviv F.C. zote za nchini humo, ipo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Novatus alisema lilikuwa jambo jema kwake kufunga japo aina ya matokeo ambayo walikumbana nayo hayakuwa rafiki.

“Sio mbaya kuambulia pointi moja kuliko kutoka patupu, tulipambana kuhakikisha tunashinda mchezo lakini mambo hayakwenda vile ambavyo tulitarajia, tunahitaji kusogea nafasi za juu na si vinginevyo,” alisema.

Ndani ya michezo 19 ambayo wamecheza hadi sasa, Beitar Tel Aviv wa-mejikuta waki-kusanya pointi 17, wapo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa timu 16 na wanachungulia kaburi.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA FEI TOTO KURUDI TENA YANGA...NABI AMALIZA UBISHI....ATOA MSHARTI YAKE...