Home news HUKU USAJILI WAKE UKINGOJEWA KWA HAMU…CHAMA AIBUKA NA KUTOA KAULI TATA…

HUKU USAJILI WAKE UKINGOJEWA KWA HAMU…CHAMA AIBUKA NA KUTOA KAULI TATA…


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chama โ€˜Triple Cโ€™ ameendelea kuwaweka njia panda wadau wa soka nchini kufuatia tetesi zinazoendelea kuwa, huenda akarejea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Chama ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa nchini kwao Zambia kwa mapunziko, amekua anahusishwa na mpango wa kusajiliwa Simba SC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, ambacho kitafikia kikomo Januari 15.

Kiungo huyo amesema: โ€œKama ambavyo Simba walikubaliana na RS Berkane nikaondoka kwao, nadhani unahitajika muda mwingine wa kufanya uamuzi kama huo kutambua kama nitakuja Tanzania au kubaki kule Morocco.โ€

Chama aliuzwa RS Berkane mwishoni mwa msimu uliopita akitokea Simba SC, lakini taarifa zinaeleza kuwa mazingira ya Morocco yamekua magumu kwake, hivyo amelazimika kuvunja mkataba wake na wakati wowote atarejea Msimbazi.

SOMA NA HII  AL HILAL YAWASILI BONGO,SABABU ZA SIMBA SUPER CUP ZAWEKWA WAZI