Yanga SC

KISA YANGA KUPOTEZA KOMBE…KAZE AVUNJA UKIMYA …AFUNGUKA ALIVYOLAZIMIKA KUMPANGA JOHARA…

admin January 12, 2022 3:19 pm


Kocha msaidizi wa Young Africans Cedric Kaze ametoa sababu za kufanya maamuzi ya kumtoa Mlinda Lango Aboutwalib Mshery na kuingia Erick Johora katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC.

Kaze ametoa sababu hizo kufuatia lawama za baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Young Africans ambao walionesha kuchukizwa na maamuzi hayo, huku wakiamini yalichangia kikosi chao kufungwa kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati.

Kaze amesema maamuzi aliyoyachukua yalikua ya kawaida, na siku zote yamekua yakifanywa na makocha wengi duniani, na kilichotokea ni sehemu ya matokeo ya mchezo wa soka.

Amesema Mlinda Lango Johora amekua akifanya vizuri kwenye mazoezi hasa uokoaji wa mikwaju ya Penati, hivyo aliamini engeweza kuisaidia Young Africans kwenye mchezo huo, lakini bahati haikuwa kwao.

“Ni mabadiliko ya kawaida tu, Johara alifanya vizuri sana kwenye mazoezi, tulifanya mazoezi ya penalti na akaonekana kuwa vizuri ndio msingi wa mabadiliko yale,” amesema Kaze.

Tayari kikosi cha Young Africans kimesharejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

BAADA YA YANGA KUTEMA KOMBE LA MAPINDUZI ..KAZE AFUNIKA USO CHINI..ATAJA WACHEZAJI WALIOMFELISHA… KISA WACHEZAJI WA MAJARIBIO..MSEMAJI SIMBA ATUPA KIJEMBE YANGA…ADAI HUO NI MFUMO WAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply