news

HUU HAPA UKWELI KUHUSU ISHU YA FRAGA KUIANDIKIA BARUA SIMBA BAADA YA KUPONA …ATAJA MAAJABU..

admin January 25, 2022 4:31 pm


Kiungo kutoka nchini Brazil Gerison Fraga Vieira ameendelea kuonesha mapenzi na klabu ya Simba SC ambayo aliitumikia kwa misimu miwili.

Fraga aliyesajiliwa Simba SC 2019 akitokea India, ameandika barua ya wazi kwa Mashabiki, Wanachama na Uongozi wa klabu hiyo ya shukurani kwao, kufuatia ushirikiano waliomuonesha kipindi chote alichocheza Simba SC.

Kiungo huyo ambaye alisitishiwa mkataba wake baada ya kuumia goti akiwa kwenye majukumu ya kuitetea Simba SC, ameandika: Barua kwa mashabiki na wanasimba

Tuliishi wakati pekee tukiwa pamoja. Ninaweza kusema kwa uhakika kwamba nyakati za kipekee nilizopata katika soka ni Dar es Salaam.

Nilipofikia, nilikuta uwanja uliojaa mashabiki wenye shauku kubwa, ambao walikuwa karibu na mimi tangu dakika ya kwanza.

Mlitushangilia, mlituunga mkono, kusherehekea na kulia pamoja nasi. Ndio maana wakati huu ni mgumu sana kwangu.

Nawapa barua hii na kusema “tutaonana baadaye”. Nashukuru kwa yote ambayo Simba imeniandalia mimi na familia yangu kwa miaka hii ya kimaajabu.

Asante kwa kushiriki pamoja katika maumivu yangu na kwa kunipa moyo ili kunisaidia katika ahueni hii.

Nipo Nje ya uwanja huku Brazil, lakini nyie mlinifanya nijihisi kama nipo Dar es Salaam muda wote.

Nitatangaza klabu yangu mpya hivi karibuni, lakini tambueni kuwa Siimba ni sehemu ya maisha yangu.

BARBARA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA NAMNA WANAVYOPIGWA VITA NNJE YA UWANJA..AITAJA TFF.. MASTAA YANGA WACHOTA SH 265…GSM WAAMUA…SIMBA WAIVIMBIA..JEURI YAO HII HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply