Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO..NYOTA 10 WA YANGA KUKOSEKANIKA…MAKAMBO AKIMBILIA KWAO ‘KUJIBUSTI’…

KUELEKEA MECHI YA KESHO..NYOTA 10 WA YANGA KUKOSEKANIKA…MAKAMBO AKIMBILIA KWAO ‘KUJIBUSTI’…


KIKOSI cha Yanga SC kitashuka tena uwanjani Jumamosi ya Januari 29, 2022 kucheza na klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza katika mchezo wa kombe la shirikisho la Azam.

Awali, mchezo baina ya Yanga SC Vs Mbao FC ulipangwa kuchezwa katika uwanja wa michezo wa Benjamin W. Mkapa uliopo manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mchezo baina ya Yanga SC na Mbao FC, sasa umepelekwa jijini Mwanza katika dimba la CCM Kirumba.

Sababu ya kuhamishwa kwa mchezo huo kutoka uwanja wa michezo wa Benjamin Mkapa ni kile kilichodaiwa uwanja huo kuwa kwenye matumizi mengine siku ya Jumamosi.

Kuwakosa wachezaji 10.

Kuelekea mchezo huo wa kombe la shirikisho la Azam, Yanga SC inatarajia kuwakosa wachezaji wake 10 kwa sababu mbalimbali.

Wachezaji wawili wa Kikongo Djuma Shabani na Yannick Bangala Litombo wenyewe watakosekana katika mchezo huo kwa kuwa wapo katika majukumu ya timu ya taifa huko Bahrain.

Mchezaji mwingine wa Kikongo katika kikosi cha Yanga SC, Herithier Ebenezer Makambo na yeye atakosekana katika mchezo huo baada ya kuomba ruhusa kwenda nchini kwao Kongo DR kushughulikia matatizo ya kifamilia.

Wachezaji Feisal Salum Abdallah, Yusuf Athuman, Yacouba Sogne, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘ Ninja’ , na Denis Nkane wapo kwenye uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo dhidi ya Mbao FC kwa sababu ya kusumbuliwa na majeraha.

Mchezaji wa 10 ambaye ataukosa mchezo baina ya Yanga SC Vs Mbao FC ni Mganda Khalid Aucho ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Ikumbukwe kuwa, mlinda mlango namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra amekosekana katika kikosi cha Yanga SC kwa zaidi ya wiki 3 kwa kuwepo kwenye majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Mali katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika zinazoendelea huko nchini Cameroon.

SOMA NA HII  KWA HILI LA MUDATHIRI...FEI TOTO BORA ASIRUDI TENA YANGA...NABI AANZA KUELEWA SHOW...