KOCHA Mkuu wa Kikosi cha Yanga, Mohamed Nabi amesema amewapiga marufuku wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo kuzungumzia matokeo mabovu ya mahasimu wao Simba Sc ambayo wamekuwa wakiyapata katika mechi zao za hivi karibuni na badala yake wajikite katika michezo yao na kuhakikisha wanashinda.
“Nimewaambia wachezaji sitaki kusikia hata wanazungumza ishu za Simba kwani matokeo yao hayatuhusu na nimewataka wazingitie na kufikiria zaidi mechi zetu zinazotukabili.
“Nimewaambia kabisa nikimkuta mchezaji yeyote anafanya hivyo au mtu yeyote katika benchi langu la ufundi akiijadili Simba au timu nyingine juu ya matokeo yao nitawapa adhabu zilizopo kwenye miongozo yao ya kazi.
“Yanga tuna mechi zetu ambazo sasa zitazidi kuwa ngumu, nimewaambia kuanzia sasa kila mchezo utakaokuwa mbele yetu utakuwa ni sawa na fainali ngumu ambazo ni lazima tuzishinde,”- Mohamed Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga Sc.
Simba katika michezo mitatu ya mwisho ya Ligi ameyeyusha dakika 270 bila kufunga bao wala kushinda huku akifungwa mechi mbili, ya Mbeya City na ile ya Kagera na kutoa sare mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.