Home news HUYU HAPA GABADINHO MHANGO…MMALAWI MASHINE YA MAGOLI AFCON…SENZO AFUNGUKA KUMSAJILI YANGA…

HUYU HAPA GABADINHO MHANGO…MMALAWI MASHINE YA MAGOLI AFCON…SENZO AFUNGUKA KUMSAJILI YANGA…


Nyota wa klabu ya Orlando Pirates, Gabadinho Mhango ametupwa nje katika michuano ya kombe la mataifa Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Malawi.

Licha ya kutupwa nje katika michuano hii Gabadinho ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi mpaka kufikia hatua ya robo fainali kutoka katika ligi ya ndani. Kipindi cha dirisha dogo la usajili nyota huyu kutoka Malawi aliwindwa sana na klabu ya Yanga.

Gabadinho amekuwa ni mchezaji hatari katika michuano hii ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON). Mpaka timu yake ya taifa ya Malawi inatolewa katika michuano hii Gabadinho amefanikiwa kufunga magoli matatu.

Ameweza kutolewa lakini binafsi amejiwekea rekodi nzuri katika michuano hii mikubwa barani Afrika. Malawi walitolewa na timu ya taifa ya Morocco ambayo moja kwa moja imetinga hatua ya robo fainali.

Michuano ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa kuna mataifa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kwa sasa yanaonekana kufanya vizuri mfano mzuri ni taifa la Gambia

Lakini pia kuna mataifa ambayo yalikuwa yanapewa kipaumbele kuwa yanaweza kufanya vizuri katika michuano hii lakini hayajaweza kufanya vizuri mfano mzuri ni taifa la Algeri ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hii.

Malawi wametolewa katika michuano hii lakini ukiangalia kundi lao lilivyokuwa wamejitahidi sana mpaka kufika katika hatua ya robo fainali. Kitendo cha klabu ya Yanga kutaka kumsajili Gabadinho inakuonesha ni jinsi gani walivyojipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano yote watakayo shiriki.

Kuna uwezekano mkubwa sana klabu msimu ujao klabu ya Yanga ikaenda kucheza michuano ya kimataifa kwahiyo bado wanaweza kumshawishi Gabadinho kutua Bongo.

Kama Yanga watampata mchezaji huyu kwa msimu ujao anaweza akawasaidia sana katika michuano ya kimataifa. Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Yanga Senzo Mazingiza tayari alisha sema kuwa kwa sasa klabu ya Yanga inaweza kumsajili mchezaji yoyote ambaye mwalimu Nabi ataonesha nia ya kumuhitaji. Kwahiyo hata Muhango Gabadinho anaweza kutua Jangwani.

SOMA NA HII  TIMU YA MSUVA UARABUNI YAMNYATIA MAYELE...WAARABU KUTUMA OFA NONO...