Home Yanga SC YANGA NAO KUSHUSHA BASI JIPYA

YANGA NAO KUSHUSHA BASI JIPYA

 


BAADA ya CEO wa Simba Barbara Gonzalez kuweka wazi mipango yao ya kutumia basi lao jipya, uongozi wa Yanga nao umejibu mapigo kwa kuweka hadharani kuwa nao watashusha basi jipya na kali zaidi ya lile la Simba.

Simba na Yanga zote zinamiliki magari aina ya Yutong ambayo walinunuliwa na moja ya kampuni iliyokuwa ikiwadhamini klabu hizo mwaka 2012 ambayo wameyatumia kwa zaidi ya miaka 8.

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa ni kweli klabu hiyo ipo katika mpango wa kununua basi jipya, na la kisasa ambalo litakuwa bora zaidi ya lile la Simba ambalo limekuwa likienea mitandaoni.

β€œYanga tupo katika mpango wa kushusha basi jipya kali kuliko lile TATA la wenzetu, sio kwamba mpango huu ni baada ya kuona wenzetu wameanza mchakato huo, hapana huu ni mpango wetu wa muda mrefu ambao tumekuwa nao.

β€œHivyo wapenzi wa Yanga wanatakiwa kutulia kwani tutashusha basi jipya na kali kwa ajili ya kikosi chetu wanapokuwa katika safari zao za hapa na pale,” amesema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HAYA MALIPO UBINGWA PAWEKWA WAZI