Home Simba SC BARBARA AFICHUA KINACHOIBEBA SIMBA

BARBARA AFICHUA KINACHOIBEBA SIMBA

OFISA mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa moja ya vitu ambavyo vimefanya wafanye vizuri kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni uwezo wao wa kuwachambua wapinzani kabla ya kukutana nao.

Barbara alisema kwa msimu huu alimua kuwekeza kwenye kutafiti wachezaji hatari wa timu pinzani na timu kwa ujumla, ndiyo maana akamuajili mtu maalumu kwa ajili ya kazi hiyo huku mitandao ikiwa ni njia nyingine ambayo amekuwa akiitumia na kupata majibu chanya ambayo yanawasaidia.

Barbara amesema mpira ni sayansi kubwa ambayo inahitaji utafiti wa kina ili kupata kitu ambacho unakihitaji, ndiyo maana kuna wakati imekuwa rahisi kuona wachezaji kama, Luis Miquissone na Clatous Chama kucheza kwenye mfumo fulani kulingana na utafiti waliofanya.

“Nilishawahi kusema sehemu fulani kuwa msimu huu mimi nimewekeza zaidi kwenye tafiti ‘analysis’, ili kuweza kubaini uwezo wa mpinzani na mchezaji gani hatari kwa mpinzani wetu, ndiyo maana niliajili mtu wa kufanya hiyo kazi na wakati mwingi nilikuwa natumia mitandao.

“Mpira unaendeshwa na sayansi na unahitaji sayansi ili kuchambua masuala, kwahiyo kwa kutumia analysis za mtu wetu unaweza kujua namna ya kupanga na kuelekeza wachezaji wako wacheze namna gani, unaweza kumwambia Kapombe, Joash cheza hivi kwa sababu huyu unayekabana naye ni mtu wa namna gani,” amesema Barbara.



SOMA NA HII  SIMBA WANA NAFASI YA KUPINDUA MEZA KIBABE, KOCHA AWATAJA WACHEZAJI HATARI