Home CAF KOCHA AL AHLY AUKUBALI MZIKI WA SIMBA

KOCHA AL AHLY AUKUBALI MZIKI WA SIMBA

 


LICHA ya klabu ya Al Ahly kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC, kocha mkuu wa timu hiyo, Pitso Mosimane ameukubali mziki wa Simba na kusema kuwa anaiona timu hiyo ikifika mbali zaidi msimu huu katika mashindano hayo.

Simba ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya timu hiyo katika mchezo wa mwisho wa kundi A la ligi ya mabingwa Afrika, ambapo mchezo wa kwaza ambao ulifanyika Dar es Salaam Simba ikiwa mwenyeji ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika Kocha Mosimane amesema kuwa licha ya timu yake kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Simba lakini anaamini kuwa, Simba imejipanga kufanya vizuri katika mashindano hayo msimu huu kutokana na kuonyesha ukomavu mkubwa katika michezo yote ya kundi hilo ambalo wamecheza.

“Tumefanikiwa kuibuka na ushindi tukiwa nyumbani, haukuwa mchezo ambao ulionekana utakuwa wa ushindani, lakini ndani ya uwanja kila mtu kashudia jinsi gani ulikuwa mchezo mzuri na wa mipango kwa timu zote, wachezaji wangu wamefanya kazi kwa ubunifu wa kiwango kisichopimika, nafahamu tunahitaji nini msimu huu.

“Simba wameonyesha upinzani mkubwa katika kundi letu, wameongoza na wanastahili, nawapongeza kwa ambacho wamekifanya ni kitu kikubwa sana kwa maendeleo yao ya mpira, wanaweza kuyafikia malengo yao kwa kufika mbali zaidi katika mashindano haya msimu huu,”alisema kocha huyo.

Simba wamefanikiwa kuongoza kundi A mara baada ya kukusanya pointi 13 huku Al Ahly wao wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 11, AS Vita katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 7 huku Al Merrikh wao wakishika nafasi ya mwisho wakiwa na pointi 2.

SOMA NA HII  IMEFICHUKA....KUMBE MKATABA WA KOCHA MPYA SIMBA UNAVIPENGELE HIVI 'KUNTU'....ALAZIMISHWA KUFANYA KAZI NA MATOLA..