Home news ILE ISHU YA DJUMA NA BANGALA KUTIMKA YANGA IKO HIVI…

ILE ISHU YA DJUMA NA BANGALA KUTIMKA YANGA IKO HIVI…


MASTAA wa Yanga, Djuma Shaaban na Yannick Bangala juzi Jumanne saa tisa kamili alfajiri walipanda ndege kurejea nyumbani kwao DR Congo tayari kwa kujiunga na timu ya taifa ya nchini kwao.

Hiyo ikiwa ni saa chache tangu mastaa warejee jijini Dar es Salaam wakitokea Arusha walipokwenda kuvaana na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Sheikh Amri Abeid mkoani huko.

Katika mchezo huo wa ligi, Yanga ilifanikiwa kuwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 ambalo lilifungwa na Dickson Ambundo akipokea pasi ya Fiston Mayele kabla ya kufunga.

Djuma na Bangala wamerejea nyumbani kwao Congo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Bahrain.Sasa rasmi timu hiyo itakawakosa wachezaji wake hao wawili katika mchezo ujao wa Kombe la FA watakaocheza dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumamosi hii kwenye

Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Wachezaji hao Jumamosi iliyopita walitangazwa kuwepo katika orodha ya wachezaji 25 wa timu hiyo wataokwenda kucheza mchezo huo wa kirafiki.

Nyota hao wawili watakwenda kucheza mchezo huo maalum wa kujiandaa kutafuta nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari Mosi, mwaka huu na wachezaji hao watakuwepo sehemu ya kikosi hicho.

Wachezaji hao tangu wajiunge na Yanga wamekuwa tegemeo na uhakika wa kuanza katika kikosi cha Nabi kinachowania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

SOMA NA HII  SIYO LEVO YENU...SIMBA HII NI NEXT LEVEL..MORRISON GUMZO AFRIKA..KIUNGO FUNDI APIGWA KISU YANGA..