Home news TAARIFA ZA NDANI….SIMBA WARIDHIA KUMKATA WAWA…SHIBOUB APEWA MKATABA..PABLO AKUNWA…

TAARIFA ZA NDANI….SIMBA WARIDHIA KUMKATA WAWA…SHIBOUB APEWA MKATABA..PABLO AKUNWA…


TAYARI uongozi wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’umefikia makubaliano ya kuachana na beki Muivory Coast, Pascal Wawa ili ampishe kiungo raia wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub ambaye kiwango chake kimeonekana kumvutia Kocha Mkuu, Pablo Franco raia wa Hispania.

Wawa alijiunga na Simba Julai 1, 2018 akitokea Al Merreikh ya Sudan iliyomsajili kutoka Azam FC msimu wa 2015/2016 mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Shiboub amerejea Simba akiwa mchezaji huru, huku klabu hiyo ikisema amekuja kufanya majaribio katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Kumbuka aliwahi kuichezea Simba msimu wa 2019/20, kisha akatimkia CS Constantine ya Algeria. Taarifa ambazo imezipata gazeti la Spoti Xtra, zinasema kwamba, licha ya viongozi kuficha Shiboub yupo nchini kwa majaribio, lakini ukweli tayari bodi yao kupitia kamati ya usajili imeshamkata Wawa kwa siri.

Mtoa taraifa huyo alisema kuwa Shiboub tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa siri na rasmi atatambulishwa kati ya Desemba 9 na 10, mwaka huu.

Aliongeza kuwa, amepewa mkataba huo mfupi wa mwaka mmoja kwa ajili ya benchi la ufundi la timu hiyo, chini ya Kocha Pablo kuangalia kiwango zaidi.

“Upo uwezekanao mkubwa wa Shiboub kuongezewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja na kufikisha miwili, lakini kamaakionesha kiwango bora.

“Hiyo ni baada ya hivi karibuni mara kutua nchini kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye sharti la kuongezewa mwingine kama atalishawishi benchi la ufundi kwa kiwango bora.

“Na jina la Wawa litaondolewa katika usajili huo wa dirisha dogo, hivyo muda wowote uongozi utatangaza kuachana na beki huyo ambaye hivi karibuni amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alizungumzia usajili hivi karibuni kwa kusema kuwa: “Kila kitu kinachohusiana na usajili tumepanga kutangaza hivi karibuni, licha ya kupokea ripoti ya kocha ilitoa mapendekezo ya wachezaji wa kusajiliwa na kuachwa katika dirisha dogo.”

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIIALIKA VIPERS YA UGANDA ...SINGIDA BIG STARS WAIALIKA TIMU HII KUBWA AFRIKA KWENYE SIKU YAO...