Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba imeendelea na kupata matokeo mabovu katika michezo yake ya Ligi Kuu NBC Tanzania bara, baada ya kukutana na kichapo cha goli 1 kwa bila kutoka kwa Kagera Sugar.
Simba wamecheza mchezo wake wa tatu na kuambulia alama 1 pekee katika michezo yake hiyo 3. Ifahamike kuwa Simba wamecheza michezo hiyo.
Mchezo wa kwanza ni dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine na kukubali kichapo cha goli moja kutoka kwa Mshambuliaji Paul Nonga. Mchezo wa pili Simba walicheza na Mtibwa Sugar na kupata suluhu ya bila kufungana.
Lakini katika mchezo wake wa tatu, Simba wamecheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera na kujikuta wakifungwa goli 1 kutoka kwa mchezaji wao wa zamani Khamis Kiiza Diego. Baada ya matokeo hayo maneno mengi yamezungumzwa juu ya Simba, lakini ukweli wote ni huu.
Kwanza kabisa, Wachezaji wa Simba wanacheza mpira kwa presha kubwa hata Kocha Pablo Franco Martin pia na yeye yupo na presha kubwa, Jambo ambalo limeifanya timu ipitie wakati mgumu katika michezo yake.
Katika kudhirisha kwamba Simba wanacheza kwa presha kubwa zaidi hii imeonekana kwa Wachezaji kama Mzamiru Yassin ambaye alipata nafasi ya kufunga goli lakini kutokana na presha hiyo akashindwa kufunga, Mfano mwingine ni Shomari Kapombe na yeye alipata nafasi ya kufunga, lakini akashindwa kufanya hivyo pia.
Kocha Pablo Franco Martin pia ameonekana pia anapresha kubwa hata ya kupanga kikosi kwani ameshindwa kabisa kuwa na kikosi cha kwanza. Kila mchezo utakuta Kocha Pablo Franco, anaingia na kikosi kipya Jambo ambalo pia linachangia hata Simba kushindwa kuwa na Muunganiko mzuri uwanjani.
Endapo Viongozi wa Simba watashindwa kukaa na timu yao kwa sasa na kuwatuliza presha waliyokuwa nayo basi waelewe kabisa hali itazidi kuwa mbaya kwani wanaenda katika mashindano ya Kimataifa ambayo wanapaswa kwenda kufanya vizuri tofauti na hapo watatia aibu kwenye michezo.