Habari za Yanga
Habari za michezo

PAMOJA NA KUCHAPWA JUZI…KIUNGO WA BAMAKO AITAJA YANGA NA MAYELE…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin March 10, 2023 7:28 pm

Kiungo mahiri wa AS Bamako ya Mali, Ibrahim Sidibe amemtaja Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga Mayele, kuwa sababu ya kikosi chao kushindwa kufurukuta kwenye mchezo wa Mzunguko wa nne wa Kundi C, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

AS Real Bamako ilikubali kichapo cha 2-0 mbele ya Yanga juzi Jumatano (Machi 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufifisha matumaini ya timu hiyo ya mjini Bamako-Mali kufuzu Hatua ya Robo Fainali.

Sidibe amesema kitendo cha wao kuruhusu bao la mapema la Mayele dakika ya nane ya mchezo kilichangia kuwatoa mchezoni licha ya kucheza vizuri.

“Lengo letu lilikuwa ni kulinda kwanza huku tukishambulia kwa tahadhari kwani tuliamini hii ni silaha kubwa kwetu kwa sababu tunacheza ugenini ingawa jitihada zake binafsi zilifanikiwa.”

“Kiujumla tulicheza vizuri isipokuwa makosa binafsi na matumizi mazuri ya nafasi kwa wapinzani wetu yaliweza kutugharimu hivyo kutuweka kwenye mazingira mabaya ya kufuzu hatua inayofuata.” amesema Sidibe

AS Real Bamako imeendelea kubaki mkiani mwa Kundi D ikiwa na alama zake 02, huku Yanga ikiwa ya pili na alama 07, wakati US Monastir ya Tunisia ikiwa timu ya kwanza kufuzu kutoka kwenye Kundi hilo baada ya kufikisha alama 10.

TP Mazembe ya DR Congo ambayo ilichapwa na US Monastir kwa bao 1-0 inashika nafasi ya tatu.

AHMED ALLY:- KIKOSI CHA PILI CHA SIMBA KWA MTIBWA NDIO KIKOSI CHAO CHA KWANZA…. WAKALA AFUNGUKA A-Z FIGISU ALIZOPIGWA KUHUSU ISHU YA ADEBAYOR KUKIPIGA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply