Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

WAKALA AFUNGUKA A-Z FIGISU ALIZOPIGWA KUHUSU ISHU YA ADEBAYOR KUKIPIGA SIMBA…

admin March 10, 2023 7:37 pm

Wakala wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Niger Victorien Adebayor amefunguka kwa mara ya kwanza namna alivyojitahidi kuhakikisha mchezaji wake anacheza soka la Bongo msimu huu 2022/23.

Adebayor alionesha kiwango kikubwa akiwa na US Gendamarie ya nchini kwao Niger, wakati ikishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu uliopita, akifunga mabao sita.

Wakala wa Mshambuliaji huyo amesema dhamira yake kubwa ilikua ni kufanya Biashara na Simba SC ya Tanzania ambayo ilionesha nia ya kumsajili, lakini Shirikisho la Soka nchini Niger liliingilia kati na kumpeleka RS Berkane ya Morocco.

Amesema Shirikisho la Soka la Niger kupitia kwa Rais Djibril Hima Hamidou, lilifikia hatua ya kufanya udanganyifu ambao hakutaka kuuweka wazi, ili kufanikisha Adebayor anatimkia Morocco.

“Nilitaka kumleta Victorien Adebayo Tanzania acheze Simba SC lakini Rais wa shirikisho la soka la Niger alifanya udanganyifu, walichukua pesa za Berkane halafu hivi sasa wamemucha kijana anahangaika peke yake, nina niwezalo kumuondoa kijana RS Berkane,” amesema wakala wa Adebayor.

Tangu Adebayor asajiliwe RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu 2022/23 ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja.

Taarifa zinaeleza kuwa Adebayor kwa sasa hana furaha ndani ya klabu hiyo, na amekuwa akishinikiza kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

PAMOJA NA KUCHAPWA JUZI…KIUNGO WA BAMAKO AITAJA YANGA NA MAYELE…ISHU NZIMA IKO HIVI… PAMOJA NA HALI NGUMU POLISI TZ…ZAHERA KAJIPIGA PIGA KIFUA KICHA AKASEMA HAYA KWA MABOSI ZAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply