News

YANGA WAKIZUBAA TU…MWAMNYETO HUYOOO MSIMBAZI…VIGOGO SIMBA KUKUTANA NA WAKALA WAKE LEO..

admin February 2, 2022 9:00 am


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanahusishwa na mpango wa kuanza mazungumzo na Nahodha na Beki kati wa klabu ya Young Africans, Bakar Nondo Mwamnyeto.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimethibitisha kuwa Uongozi umedhamiria kuipata saini yake huku ikifahamika kuwa leo Jumatano (Februari 02), huenda ukafanya mazungumzi na meneja wa mchezaji huyo Kasa Musa.

Simba SC pia bado wamemng’ang’aninia kiraka wa Yanga SC Kibwana Shomari ambao wote kandarasi zao zinaisha mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo Klabu ya Simba SC haijazungumza lolote kuhusu mpango huo kwa wachezaji wote wawili, zaidi ya kuendelea kuzungumza kama Tetesi katika mitandao ya kijamii.

WAKATI WENZAKE WAKIZIDI ‘KUINJOI’  YANGA….ISHU YA KIBWANA NA WENZAKE IMEFIKIA HAPA…NABI ‘ASUSIWA’… AHMED ALLY AFUNGUKA ALIVYOPATA KAZI SIMBA…AMTUPIA DONGO MANARA…ADAI WATU HAWAMKUMBUKI TENA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply