Mjasiriamali wa Morogoro Ajishindia Bajaj Kupitia Kampeni ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Kuwa Mchezoni Ushinde!
MOROGORO, Tanzania — Alex Kagesya, mjasiriamali kutoka Morogoro, sasa ni mmiliki wa Bajaj mpya baada ya kushinda kupitia kampeni ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Kuwa Mchezoni Ushinde. Ushindi wake umekuja baada ya kushuhudia mkazi mwingine wa Morogoro akikabidhiwa Bajaj, jambo lililomvutia na kumtia hamasa ya kushiriki kampeni hiyo.
Alex alipata taarifa za kampeni kupitia mitandao ya kijamii na kuona picha za mshindi wa kwanza kutoka Morogoro akikabidhiwa zawadi yake. Tukio hilo lilimfanya atambue kuwa naye angeweza kupata nafasi ya kushinda. Badala ya kubaki mtazamaji, aliamua kushiriki kampeni hiyo na kujaribu bahati yake.

Alicheza mchezo wa BALLOON kupitia tovuti ya Bahati Nasibu ya Taifa, www.nationallottery.co.tz, kwa TZS 35,000 na hatimaye kuibuka mshindi wa Bajaj. Kwa Kagesya, kile kilichoanza kama hamasa baada ya kuona mkazi mwenzake akishinda kimegeuka kuwa furaha ya kumiliki Bajaj yake mwenyewe.
Ushindi wake unaongeza jina la Kagesya kwenye orodha ya washindi wa kampeni ya Kuwa Mchezoni Ushinde, iliyoanza mwezi Mei mwaka huu na kutoa zawadi mbalimbali kwa washiriki. Zawadi hizo zilijumuisha Smartphone tano kila siku, pamoja na zawadi za kila wiki kama Soundbar, Smart TV, Tablets, Pesa taslimu TZS 1,000,000, Pikipiki na Bajaj.
Kupitia kampeni hiyo, Bahati Nasibu ya Taifa iliendelea kuwapa wachezaji nafasi ya pili ya kushinda na kuwafikia washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini. Ushindi wa Kagesya unaongeza simulizi nyingine ya mafanikio, huku ukionyesha jinsi ushindi wa mtu mmoja unavyoweza kumtia mwingine hamasa ya kushiriki na kujaribu kupata zawadi yake mwenyewe.

Makabidhiano ya Bajaj kwa Kagesya yanaashiria hatua nyingine ya mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya Kuwa Mchezoni Ushinde, iliyoanza mwezi Mei, na kuongeza furaha kwa mshindi mwingine kutoka Morogoro.
Nawe unaweza kushiriki michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa na kupata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali. Tembelea www.nationallottery.co.tz au piga *149*88#, chagua mchezo unaopenda na ucheze. Umeshuhudia wengine wakishinda. Sasa ni wakati wako kujiunga na kujaribu bahati yako!
-
Newspaper News Feature Caption
| ENGLISH | KISWAHILI |
| Alex Kagesya (right) receives the Bajaj key from Richard Kimaro, Marketing Officer at National Lottery, after winning through the Kuwa Mchezoni Ushinde campaign, which launched in May this year.
|
Bw. Alex Kagesya (kulia) akipokea ufunguo wa Bajaj kutoka kwa Bw. Richard Kimaro, Afisa Masoko wa Bahati Nasibu ya Taifa, baada ya kuibuka mshindi kupitia kampeni ya Kuwa Mchezoni Ushinde, iliyoanza mwezi Mei mwaka huu.
|
- Social Media Caption
| ENGLISH | KISWAHILI |
| 🚨 BALLOON PAYS OFF! ALEX WALKS AWAY WITH A BRAND-NEW BAJAJ!
Alex Kagesya from Morogoro is now the proud owner of a brand-new Bajaj after winning through the @nationallottery_tz Kuwa Mchezoni Ushinde campaign by playing BALLOON. YOU COULD BE THE NEXT WINNER! Play National Lottery games today at www.nationallottery.co.tz or dial *149*88#! 18+. Cheza Kistaarabu. ITHUBA ni mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa. #AminiChezaUshinde
|
🚨BALLOON IMELIPA! ALEX AONDOKA NA BAJAJ MPYA!
Alex Kagesya kutoka Morogoro sasa ni mmiliki wa Bajaj baada ya kuibuka mshindi kupitia kampeni ya @nationallottery_tz Kuwa Mchezoni Ushinde kwa kucheza BALLOON.
WEWE PIA UNAWEZA KUSHINDA! Cheza Michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa sasa kupitia www.nationallottery.co.tz au piga *149*88#! 18+. Cheza Kistaarabu. ITHUBA ni mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa. #AminiChezaUshinde |