news

WAKATI WENZAKE WAKIZIDI ‘KUINJOI’ YANGA….ISHU YA KIBWANA NA WENZAKE IMEFIKIA HAPA…NABI ‘ASUSIWA’…

admin February 2, 2022 9:00 am


BEKI kiraka wa Yanga, Kibwana Shomari na mwenzake Abdallah Shaibu ‘Ninja’, wanahesabu siku tu za kurudi uwanjani mara baada ya kupona majeraha yao.

Kibwana anayemudu kucheza beki wa kulia na kushoto, wiki mbili zilizopita alikwenda Tunisia sambamba na Ninja kwa ajili ya kufanyiwa operesheni ya majeraha yanayowasumbua.

Kurejea kwa mabeki hao kutampa upana wa kikosi Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana na kuthibitishwa na daktari wa timu hiyo, Youssef Ammar, mabeki hao watarejea uwanjani mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Februari 5, mwaka huu.

Ammar alisema mabeki hao wataanza kufanya mazoezi mepesi ya uwanjani baada ya kumaliza program ya gym wanayoendelea nayo hivi sasa.

“Kibwana na Ninja walifanyiwa operesheni ndogo ya goti ambayo itawarejesha haraka uwanjani tofauti na Yacouba (Songne) ambaye operesheni yake ilikuwa kubwa na kumfanya kukaa nje karibia miezi minne.

“Hivyo Kibwana na Ninja upo uwezekano wa kujiunga na mazoezi ya uwanjani pamoja na wachezaji wenzake hivi karibuni,” alisema Ammar.

EEHE…UMESIKIA ALICHOSEMA MUGALU HUKO SIMBA..?…AFUNGUKA A-Z YALIYOJIFICHA MOYONI… YANGA WAKIZUBAA TU…MWAMNYETO HUYOOO MSIMBAZI…VIGOGO SIMBA KUKUTANA NA WAKALA WAKE LEO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply