news

PAMOJA NA GSM KUSALIMU AMRI UDHAMINI WA LIGI KUU…AHMED AZIDI KUIPAKA ‘CHUMVI NA PILIPILI’..AJA NA HILI…

admin February 9, 2022 10:00 am


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally klabu ya Simba kwa sasa haina washabiki lialia kwa sababu simba hawaliilii lakini wana mashabiki wa kufurahia, ‘lialia timu nyingine hizo zenye maisha magumu’.

Akizungumzia GSM kujitoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara, Ahmed amesema; “Tufike mahali tuvalue thamani ya Ligi yetu, thamani ya timu zetu, unakwenda kuipa timu ya Ligi Kuu milioni 3 kwa mwezi ? Kuna wakati mwingine inakulazimu uonyeshe thamani yako.

“Milioni tatu haitoshi hata maandalizi ya machezo mmoja, achilia mbali mwezi mmoja na kama Prison huyo anayelia hana milioni tatu ni Timu ya Kushuka daraja, hatuwezi kuwa na Timu ambayo haiwezi kuwa hata na milioni tatu tutakuwa tunashindana nini sasa?

“Tumeshafahamu tulikosea wapi, zile moods za mechi tatu tumeshamalizana nazo, tumejipanga tumejua makosa yalikuwa wapi, tumejifunza kutokana na hayo makosa sasa tunaelekea mbele.

“Kwenye mechi hizi za Shirikisho huwezi kucheza kwenye uwanja kama Manungu, unacheza na watu wenye mentality, hizi ni mechi za kikubwa tunacheza kikubwa, mnaenjoy,” Ahmed Ally.

MATAJIRI YANGA WAAMUA KUFANYA KWELI ISHU YA MORRISON…WAMPA MKATABA WA KIMKAKATI…SIMBA WAKODOA MACHO.. BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHA TFF…PABLO AIVUA UBINGWA SIMBA…AGUSIA TIMU YAKE INAVYOCHEZA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply