Home news SIKU KADHAA KABLA YA KUVAANA NA WAIVORY…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA SIMBA…DILUNGA NI MAJANGA...

SIKU KADHAA KABLA YA KUVAANA NA WAIVORY…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA SIMBA…DILUNGA NI MAJANGA TU…


BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema wanatambua ugumu wa mechi ya Jumapili dhidi ya Asec Mimosas, mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Kapombe amesema wanajiandaa vilivyo kuhakikisha wanapata ushindi mnono, utakaowapa nguvu katika mechi ya ugenini.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga kuhakikisha mashabiki wetu wanaondoka na kicheko kitakachotokana na ushindani tutakaotoa” amesema Kapombe na kuongeza;

“Tunahitaji kusonga mbele zaidi, kwani Simba ndio timu pekee inayoliwakilisha taifa kimataifa.”

Simba imefanya mazoezi juzi Februari 8 jioni katika uwanja wa Mo Simba Arena, uliopo  Bunju jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo sio kikosi kizima kilichomfanya  mazoezi , kutokana program aliyoiweka kocha wa timu hiyo, Pablo Franco.

Wachezaji ambao wamefanya mazoezi katika uwanja huo ni wale walioingia katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza na ambao hawakucheza kabisa.

Mastaa hao ni Beno Kakolanya, Ally Shomari, Pascal Wawa,Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Joash Onyango, Mzamiru Yassin, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Peter Banda, Clatous Chama na Hassan Dilunga ambaye ameumia na kutolewa nje.

Mastaa ambao hawakuwepo, walipangiwa programu ya gym.

SOMA NA HII  KIGOGO TFF AFICHUA UKWELI WA MKATABA WA DUBE NA AZAM FC...'HAKUNA MIL 700 ..SIASA TUPU..."