HATIMAYE Uongozi waYanga, umelitaka benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na kocha raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, kuwasilisha mara moja ripoti ya mpango kazi unaoainisha mambo watakayoyafanya takribani wiki mbili za mapumziko kabla mechi za Ligi Kuu Bara kurejea.
Yanga bado ni vinara wa ligi, wakiwa na jumla ya pointi 36, walizozipata baada ya kucheza mechi 14 na kuvuna ushindi katika mechi 11, huku wakitoka sare tatu.
TayariYanga ipo kambini ikiendelea kujinoa kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho laAzam Sports, ambapo Februari 15 watakuwa wenyeji wa Biashara United, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Chanzo chetu kutoka ndani yaYanga, kimesema kuwa, uongozi umelita benchi la ufundi kupitia kwa mratibu wa mashindano, Thabit Kandoro