Home news WAKIWA KWENYE MBIO ZA UBINGWA …MASTAA TISA WASHTUKIWA YANGA…NABI AWATAJA..AITA KIKAO KIZITO...

WAKIWA KWENYE MBIO ZA UBINGWA …MASTAA TISA WASHTUKIWA YANGA…NABI AWATAJA..AITA KIKAO KIZITO FASTA…


KOCHA wa Yanga, Nesreddine Nabi amepania kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mapema iwezekanavyo, lakini amechunguza mwenendo wa mastaa wake kiutimamu wa mwili akashtukia kitu.

Wapo kama tisa ambao wanaumia mara kwa mara. Lakini wanaumia majeraha ambayo yamekuwa pia tatizo kwa wengine mara kadhaa.

Nabi ameamua kutumia muda wake wa ziada kuitisha kikao na uongozi pamoja na wataalam wa tiba kuona jinsi ya kupambana na tatizo la wachezaji hao ili wasimtoe kwenye reli ya kuwania ubingwa.

Nabi amesema kwamba kama kuna kitu kinampasua kichwa ni uwepo wa mastaa wake 9 ambao wanakabiliwa na majeruhi nyakati hizi za hesabu kali. Alisema hadi sasa ingawa ameanza mazoezi kiungo wake Feisal Salum bado hajamuona kama yuko sawasawa sambamba na beki wa kushoto Yassin Mustapha ambaye naye amepata maumivu mara kadhaa.

Wengine ni pamoja na beki Kibwana Shomari,Abdallah Shaibu Ninja na Yacouba Songne ambao walifanyiwa upasuaji nchini Tunisia ambao bado wako katika programu maalum ya kupona huku Yusuf Athuman na beki Dickon Job nao hali zao zikiwa bado ngumu.

“Inaumiza sana kichwa hali hii lakini bado tunapambana kutafuta kujua kipi kinawakumba baadhi yao wameanza kurejea taratibu inatia imani lazima tujue kipi kinasababisha haya majeruhi ya aina hii wakati huu.

“Wapo ambao najua walihitajika kupumzika hapa kati hatukutakiwa kucheza baadhi ya mashindano lakini niliambiwa kwamba haitawezekana hilo nalo linachangia,” alisema Nabi

“Ni muhimu kukutana na kulifanyia tathimini hili tutakutana na viongozi tuweze kutafuta njia ya kuondoka katika eneo hili vinginevyo linaweza kutuharibia hesabu zetu kwenye mambo ambayo tunataka kufanikisha.”

Kwa upande wa Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija alisema ni kweli idadi ya majeruhi imeongezeka ndani ya timu baada ya Chrispin Ngushi kugundulika na tatizo ambalo linamuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita.

“Matatizo yanayowasumbua wagonjwa ni siri ya daktari na mgonjwa hauwezi kuweka wazi kinachotakiwa kufahamika sasa ni kwamba hatutakuwa na wachezaji hao kwa muda hadi watakapokabidhiwa tena chini ya Nabi,” alisema na kuongeza;

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YAO YA LIGI....FEI TOTO KAIBUKA NA HILI JIPYA KWA YANGA...

“Ngushi ishu yake ni tofauti na wengine baada ya kubaini tatizo lake imetulazimu kumpa mapumziko ya wiki sita, Nkane na Yassin ameanza mazoezi ya viungo wakati Yacouba, Kibwana na Ninja tayari wameanza mazoezi ya nguvu,” alisema Mngazija ambaye ni miongoni mwa madokta wazoefu.