ALIYEKUWA mchezaji wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni “Sonso” (29) amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa Matibabu leo Ijumaa, Februari 11, 2022.
Taarifa za awali zinasema kuwa, Sonso ambaye alikuwa beki wa kushoto akikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu. Kwa nyakato tofauti, Sonso amezitumika timu za Lipuli FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Polisi Tanzania. Pia amewahi kucheza timu ya Taifa.
Mtangazaji wa Clouds FM Prisca Kishamba ameandika kwenye ukurasa wake hivi; “Nasikitika kuwasilisha msiba wa Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Yanga SC na KMC FC Ally Mtoni Sonso. msiba umetokea hapa Hospital ya Taifa ya Muhimbili muda mchache uliopita. Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe”.
Taarifa zaidi itafuata