news

KUELEKEA MECHI YA KESHO…PABLO AINGIA BARIDI SIMBA…AIJAZA UPEPO ASEC MIMOSAS MAPEMA…

admin February 12, 2022 3:58 pm


Kocha wa Timu ya Simba, Pablo Franco akizungumza kuelekea mchezo wa Shirikisho barani Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast utaochezwa kesho uwanja wa Benjamini Mkapa amesema watahakikisha wanapambana kushinda mechio hiyo kwani maandalizi yote yako vizuri.

“Kesho tunakwenda kukutana na mchezo wa kwanza ngumu msimu huu, mchezo utakao tupa mwelekeo wetu Katika hatua ya makundi, tutakwenda kutumia maandalizi yetu vizuri kwa kuwa Asec Mimosas Ni timu nzuri, kwenye kukaba, kushambulia na mipira iliyokufa (set pieces).

“Ni mechi muhimu tukiwa na faida kuanzia nyumbani, lakini nadhani itakuwa mechi ngumu zaidi ndani ya msimu huu. Kwangu ASEC Mimosas ni timu iliyo kamilika. Tutahitaji kuwa na mchezo kamili ili kupata matokeo.

“Ninaamini tutaanza kupata mabao mengi, tumekuwa tukifanya mazoezi kuhusu ufungaji na kila kitu kitakaa sawa kuanzia mchezo wa kesho dhidi ya ASEC Mimosas. ASEC ni timu bora na ina uzoefu mkubwa,” amesema Kocha Pablo.

ASEC Mimosas tayari wameshapima Vipimo vya Covid 19 na majibu yametoka wote wako negative hakuna mwenye virus vya corona.

Takwimu zinaonyesha ndani ya michezo 5 ya ligi yao (Asec Mimosas), imepachika mabao 10 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara mbili tu.

Simba itawakosa wachezaji 5 dhidi ya ASEC Mimosas

Clatous Chama

Kibu Denis

Bernard Morrison

Chris Mugalu

Shomari Kapombe (sio 100%).

MASAU BWIRE AFUNGUKA A-Z KUUMWA HADI KIFO CHA SONSO…ADAI FAMILIA WALIINGILIA KATI…AITAJA SIMBA…. BAADA YA KUIONA ASEC MIMOSAS ILIVYO…AHMED ALLY AGUNA KISHA AKAFUNGUKA HAYA…AGUSIA KUPAKI BASI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply