News

BAADA YA KUSIKIA TETESI ZA KUSAJILIWA KWA MORRISON….YANGA WAVUNJA UKIMYA…MASHABIKI WALIPUKA HIVI…

admin February 13, 2022 12:38 pm


TANGU kuwepo kwa taarifa za kusimamishwa kwa winga wa Simba, Bernard Morrison kisha kuvuja kwa tetesi kwamba klabu yake ya zamani, Yanga ipo mbioni kumrudisha kikosini kumekuwa na maoni tofauti na wasomaji wetu.

Gazeti la Mwanaspoti limewachapishia ujumbe tofauti wa wasomaji  jinsi wanavyomzungumza nyota huyo kutoka Ghana, ila wengi wakimkataa kurudi Jangwani.

Zilipokelewa zaidi ya meseji 256 kupitia namba yetu ya 0658-376417. Ebu zisome baadhi yake…!

MORRISON ni mchezaji mzuri, ila kwa mazingira aliyoondokea ningeshauri tuachane naye. Yanga bila BM3 inawezekana.

Simon Said, Kifuru Kinyerezi

KWA mtazamo wangu naona sio wakati sahihi kwa mchezaji huyo kurudi Yanga maana hajielewi kabisa.

Shemdoe Chakale, Muhuza Tanga

KWA ninavyojua ni kwamba Yanga hawana uhitaji wa huduma ya Morrison, bali watamsajili kama kuikomoa Simba tu.

Saleh Omary wa Al Saedy, Morogoro

KWA mtazamo wangu sio sahihi kwa Bernard Morrison kurudi Yanga, maana aliondoka kwenda Simba kiutata na hata kutaka kwake kurudi ni vilevile.

Bashiru Abdallah, Sokoni Arusha

BINAFSI naona ni sahihi Yanga kutaka kumrudisha Bernard Morrison kwa kuwa viongozi wao wameona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Makwa Mlanga, Mwandiga Kigoma

KUMRUDISHA Morrison Yanga sio sahihi kabisa huyo wamuache atokomee mbali nidhamu yake mbovu sana.

Aisha Mgaya, Tanga

SIO jambo la kushangaza kama Morrison atarejea Yanga, ni hulka ya klabu zetu kufanya hivyo kwa kukomoana, ila kwa Morrison namna alivyoondoka Yanga ni vigumu sana kurudi.

Paulo Chuwa, Soko Kuu Moshi

MORRISON kurudi Yanga kwa upande wangu naona sio sahihi, kaleta vituko vingi na pia timu ipo vizuri wa-achane nae aendelee na maisha mengine nje ya Yanga.

KISA MECHI NA WAIVORY LEO….SIMBA WAHAMA KAMBI YAO KIMACHALE USIKU USIKU.. SIMBA YA MO DEWJI WAAMUA KUFANYA KWELI AFRIKA…WACHEZAJI WATENGEWA BILIONI 1.4 KAMA BONASI TU..INAANZA LEO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply